Friday, April 1, 2011

HUU NDIO UZURI WA TANZANIA

                                             




                           
Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895). Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi kuliko mlima tu ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima.
Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko takriban mnamo mwaka 1730.
Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru Peak. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kijer.:Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.
Kibo ina theluji na barafuto kadhaa ndogo.
                                                                              

No comments:

Post a Comment